Life and news about Tanzanian celebrities
Africa: 21 | Tanzania: 1 | Visits: 15 | Page Views: 8 | Links (Blogs): 187 | Links (Posts): 109
Mwisho wa wiki mwingine umewadia.Siku zinazidi kuyoyoma.Mwaka 2008 unazidi kuelekea ukingoni.Ni wakati mwingine wa kufurahi na pia kutafakari mambo mbalimbali na jinsi wiki ilivyokwenda.Kwa jinsi maisha yalivyo,mwisho wa wiki unapowadia kila mtu ana mipango yake na kila mtu ana lake la kusimulia.Leo ikiwa nzuri kwako sio lazima iwe hivyo hivyo kwa mwenzako,jirani yako nk. Kwa bahati mbaya wiki hizi mbili zilizopita(kiujumla) zimetawaliwa na habari za misiba.Imetokea ile ya ....
Jina lake kamili ni Robert Gathecha Mongi.Wengi hivi leo tunamtambua kama Bobby.Bila shaka kabisa,Bobby ni miongoni mwa wasimamizi mahiri wa shughuli(MC),watangazaji wa radio na televisheni ambao Tanzania ya leo inaweza kujivunia.Awe anasimamia shughuli,radioni au kwenye televisheni ukimsikiliza utagundua jambo moja;anaipenda kazi yake na anaifanya kwa umakini na utulivu wa hali ya juu.Pengine utulivu huo ndio uliomfanya awe ni mtangazaji wa kutegemewa katika vituo mbalimbali vya radio nchini Tanzania na ....
Baada ya kuwa ulingoni kwa mwaka mzima akiwa kama Miss Tanzania 2007,Richa Adhia(kushoto) sasa amempisha Nasreem Karim(Miss Tanzania 2008,kulia).Nini tutavuna nini mwaka huu kwenye steji ya ulimwengu(Miss World) hapo October 4 huko jijini Kiev,Ukraine?Ni jambo la kusubiri na kuona huku tukitakiana kila la kheri. Photo/Michuzi bongocelebrity ....
Sambamba na shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2008,palikuwepo pia mchakato ulioendeshwa na kampuni ya Global Publishers ili kumpata mrembo ambaye watu mbalimbali waliona ndiye mwenye mvuto zaidi ya wengine.Tutakuwa hatukosei sana tukisema kwamba zoezi hilo lilikuwa ni kama vile kutafuta mrembo ambaye ni People’s Choice.Aliyeibuka mshindi katika hilo ni mrembo Kelly Kamwelu(pichani) ambaye ndiye Miss Ilala 2008.BC inampongeza na kumtakia kila la kheri. ....
WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika(pichani) amepiga marufuku wananchi kuweka wimbo wa taifa katika simu zao za mkononi. Mkuchika alisema kufanya hivyo ni kuudhalilisha wimbo wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla kwani inapaswa kuheshimiwa mahali popote . ”Unakuta mtu ameweka wimbo wa taifa kwenye simu yake ya mkononi halafu anapopigiwa ama yuko kwenye ulevi au mahali kwingine ambako wimbo huo hauhitajiki, hakika tunaokosesha heshima ....
Haya tena,mwisho wa wiki ndio umeshawadia.Kama kawaida ya dunia na ubinadamu,imekuwa ni wiki nyingine yenye pilikapilika za aina yake.Pilikapilika za maisha wakati mwingine hufanya nijiulize swali moja;Hivi ilikuwa ni nia na dhumuni la muumba kwamba dunia au wanadamu tuwe na mahangaiko namna hii au sisi wenyewe tu ndio tume-complicate mambo?Kama jibu ni ndio,basi kwanini tusimpigie goti muumba na kumuomba atuonyeshe njia na kuweka mambo yawe “tambarare” kama ambavyo pengine ....
Zimebaki siku chache tu kabla ya Tanzania kumpata mrembo wake wa mwaka huu (Miss Tanzania 2008). Wadau wa masuala ya urembo tayari wameshaanza kukuna vichwa wakijiuliza ni nani ataibuka mshindi mwaka huu. Mashindano ya Miss World mwaka huu yanatarajiwa kufanyika tarehe 4 October huko jijini Kiev nchini Ukraine. Sasa wakati tukisubiri kumjua atakayetuwakilisha mwaka huu huko Ukraine, kampuni ya Global Publishers,wanaendesha zoezi ambalo litakuwezesha wewe msomaji na ....